Anaitwa Ritha Komba Aliyewahi Kuimba Wimbo Unaoitwa Kivulini Pako Ni wimbo mzuri sana ulioweza kubariki watu wengi sana kutokana na maudhui yake, Lakini pia leo tena ameweza kutuletea ingizo jipya kabisa na ni kazi iliyofanyika chini ya usimamizi wa studio yake inyoitwa Ritha's Records Chini ya mwaandaji mahili kabisa ndugu Kingson(Producer).
Wimbo unakwenda kwa jina la Mwanamke Wa Imani Wimbo huu kauimba maalum kwa ajili ya wanawake na mabinti wote toka Tanzania na duniani kote, Lengo kuu ni kuwatia moyo na kuwaasa wasimame imara kiimani kutokana na magumu na changamoto zote ambazo wamekuwa wakipitia katika maisha.
Ni wimbo ambao ukiusikiliza huwezi acha kuurudia tena na tena kuweza kuusikiliza. Mungu akubariki na kumbuka kuwashirikisha wengine, Kwa wale ambao wanahitaji kuwasiliana naye kwa ajili ya huduma na mialiko mbalimbali ikiwemo pamoja nahuduma za kufanya kazi studion kwake wasiliana naye kupuitia mawasiliano haya hapa chini.
Simu/WhatsApp: +255 712 496 727
Facebook: Ritha Komba
Instagram: @rithakomba
Email: rithakomba@yahoo.com au synyoritha@gmail.com
Facebook: Ritha Komba
Instagram: @rithakomba
Email: rithakomba@yahoo.com au synyoritha@gmail.com
Comments
Post a Comment